ELIMU KWANZA

ELIMU KWANZA
KWETU FEDHA SIO KIPAUMBELE.

Saturday 21 December 2013

MPE MPENZI WAKO SABABU YA KUWA NA WEWE!!!SOMA HAPA KUJUA NAZUNGUMZIA NINI.....

KARIBUNI kwenye uwanja wetu tujadiliane kuhusu mapenzi. Marafiki zangu, katika uhusiano umakini wa hali ya juu huhitajika ili uweze kuwa bora kila siku na kuufanya uhusiano wako kuwa wenye nguvu na usiotetereka! Katika hili hutegemea zaidi jinsi unavyoendesha uhusiano wako.

Ukitaka mpenzi wako akuchoke au umchoke, wewe ndiye mwamuzi, lakini pia ukitaka mpenzi asikuchoke au usimchoke wewe ndiye mwenye uamuzi kwa kuwa una uwezo wa kuyafanya yote hayo. Hebu nikuulize, umempa sababu mwenzako ya kuwa na wewe?

Saturday 14 December 2013

MAMBO YATAKAYOKUFANYA UONEKANE BORA KWA MPENZI!

NDUGU zangu, kuna ambao wapo katika uhusiano lakini hawajui mambo ya kufanya ili wawe bora kwa wapenzi wao. Mada hii itagusia pande mbili. Upande wa kwanza ni kwa wale ambao ndiyo kwanza wapo katika hatua za mwanzo kabisa na wapenzi wao na upande wa pili ni kwa wale ambao tayari wapo katika uhusiano lakini hawajui jinsi ya kuwafanya wawe bora kwa wapenzi wao.




Inawezekana wewe ukawa mmoja wao, sasa huna sababu ya kukata tamaa na kuona kuwa huna thamani tena kwa mpenzi wako. Kwa kufuatilia vyema vipengele vifuatavyo, naamini kwa namna moja au nyingine utakuwa mpya na penzi lako litazidi kudumu zaidi na zaidi.


MWANZO WA PENZI