ELIMU KWANZA

ELIMU KWANZA
KWETU FEDHA SIO KIPAUMBELE.

Tuesday 15 October 2013

UJUWE UTUMWA WA NGONO


WATU wengi ni watumwa wa ngono bila wenyewe kujua. Lakini ubongo una kazi gani katika utumwa wa ngono? Ni njia gani zilizopo katika kupambana na uraibu na kurejea katika hali ya kawaida pamoja na kujizatiti na kujihakikishia tena kuwa na maisha ya mapenzi yaliyo bora? Kitu kilicho bora, ninaamini ni kwenda hatua kwa hatua katika kulielezea tatizo hili.


Utumwa wa Ngono ni nini?
Mapenzi ya kushurutishwa, yale ya lazima, ambayo mtu analazimika kufanya bila kufuata taratibu, yaani ile tabia ya kutaka kufanya mapenzi au vitendo vya ngono kila wakati, kila mahali na mtu yeyote, ni uraibu na utumwa, tena ni tatizo ambalo linaweza kudhibitiwa. Kwa maana nyingine uraibu wa ngono ni ile tabia ya mtu kupenda kufanya mapenzi kila wakati, kila mahali, na kutotosheka na mapenzi ayapatayo.
Watu wa aina hii wako wengi, wengine hupendelea vitu fulani katika kukidhi kiu zao za mapenzi, kama vile kupiga punyeto (kujichua: kwa mwanamke na mwanaume na kuna wanawake ambao siku hizi wanapenda sana kutumia viungo bandia vya kiume ili kukidhi kiu zao, hasa wasagaji), kutazama picha za ngono, kuchungulia watu wakifanya mapenzi na mambo mengine kadha wa kadha.
Wapo pia watu; wanawake kwa wanaume, ambao hata kama wako na wapenzi wao huwa hawafikii mshindo mpaka ama wakumbuke picha ya ngono waliyopata kuiona au wamfikirie mtu ambaye wanampenda sana na wangetamani kufanya naye mapenzi.
Watu kama hawa, bila kuvuta hisia kama hizi katu hawawezi kuridhika, na mara baada ya kufikia mshindo huwa hawawezi kabisa kuendelea kufanya mapenzi kwa ngwe nyingine na hujiona kama wanajilazimisha tu!
Mapenzi bora na yanayonoga ni yale yenye mvuto na hisia. Haya hutoa nafasi ya kufurahia uhusiano ulio bora zaidi na wenye mvuto yakini. Lakini kwa baadhi ya watu, kuna msukumo wa lazima ambao huwalazimu kujiingiza katika vitendo vya ngono vilivyokithiri na visivyofaa.
Utumwa wa ngono huharibu maisha ya kawaida ya mapenzi ya mhusika. Watu walioraibiwa na ngono hawawezi kudhibiti au kuahirisha hisia zao za ngono pamoja na matendo yao. Wataendelea na vitendo vyao viuvo vya ngono, wakihangaika kuzifurahisha hisia zao za mapenzi kwa gharama yoyote ile, wengine kama siyo kujichua, huishia hata kubaka watoto, na wanaume wengine hata kama wanazo fedha, unaweza kuwakuta wakisaka changudoa na hata mashoga, kutegemeana na wapi hisia zake zinakompeleka.
Wanaume wengine, japokuwa wako kamili, lakini hisia zao zinaweza zikawapeleka kutaka kulawitiwa, nao hufanya hivyo, na ndiyo maana unaweza kukuta katika jamii mtu fulani anaelezwa kwamba ana tabia za kishoga ukakataa, au mwingine ana mumewe lakini anatamani sana kufanya mapenzi na mwanamke mwenzake, yaani wanasagana!
Kwa watu wengine walioraibiwa na ngono, suala la kutimiza haja zao za ngono huwa ndilo linachukua nafasi kubwa katika maisha yao, na ni muhimu kuliko familia, marafiki, au hata kazi zao.
Nimeshakutana na watu wa aina mbalimbali wakati nikifanya uchunguzi wangu, na baadhi ya wanaume walikuwa na mtazamo tofauti. Yupo mmoja ambaye ana familia yake, lakini hupendelea kuwahonga baadhi ya vijana ili wakamlawiti, yupo mwingine aliye na mke mzuri sana, lakini anasema kwamba pamoja na kufanya mapenzi na mkewe, lakini lazima kwa wiki moja atafute shoga afanye naye mapenzi, mwingine anasema kwamba, lazima atafute changudoa, na mwingine yeye anasema wazi kwamba, anapendelea zaidi kufanya ngono na wasichana wa kazi, yaani mayaya (house girls); awe kwake au kwa jirani yake, ilimradi ni yaya, basi kwake ni halali!
Zaidi wapo wengine ambao wanasema kwamba, kabla ya kufanya mapenzi na wake zao ni lazima waingia bafuni wakajichue (kupiga punyeto - masturbation) ndipo wawaingilie wake zao.
Wanawake nao wana mambo yao, wapo ambao pamoja na kupatiwa kila kitu na waume zao, lakini huwa hawatosheki mpaka wafanye ngono na vijana wao wa kazi au vijana hohehahe na wao ndio hugharamia kila kitu.
Wapo ambao hupendelea kusagana na wanawake wenzao, na wapo ambao huwa hawatosheki kabisa na penzi la mume mmoja. Wanataka kujaribu uwezo wa kila mwanaume.
Wengine – wanaume kwa wanawake – wanasema hawawezi kufanya tendo la ndoa mpaka kwanza waangalie mkanda wa ‘bluu’ (picha za ngono). Hizi, wanasema, huwasisimua na kuwapandisha ashki na ndipo hupata fursa ya kuingiliana.
Huu wote ndio unaoitwa uraibu, ama utumwa wa ngono, ambao nina imani kila mmoja wetu anao au alipata kuwa nao bila mwenyewe kujiujua.


Ubongo na Utumwa wa Ngono
Ubongo huitikia na kuongoza elementi kubwa za mfumo wa ndani wa taarifa za kemikali za mwili wa binadamu. Msisimko wa mahaba huchochea mwenendo mzima wa mfumo mkuu wa neva, ukiibua mabadiliko kadhaa ya mwili.
Matumainio ya raha huongeza uzalishaji wa homoni, huongeza kasi ya mapigo ya moyo, huongeza msukumo wa damu na kuimarisha umakini wa neurone. Sitiari ya "kemia" baina ya watu wawili hubadilika na kuwa biokemia kwa uhakika, hasa kemikali yaphenylethylamine (PEA) inapoonekana kwenye ubongo.
PEA inahusika na msukumo na nguvu za kumwezesha mtu aangukie mapenzini na kutekwa. Viwango chipukizi vya kemikali hii huleta matokeo ya ongezeko la raha na mpagawisho (intensified excitement & euphoria).
Watumwa wa ngono hutegemea zaidi hamasa ya kimwili na kisaikolojia inayochangiwa na 'dawa ya mapenzi' ya PEA iliyo ndani ya ubongo.


Fahamu Ulazima wa Ngono
Watu wengi walioraibiwa katika mapenzi walipatwa kukumbwa na mikasa ya kunyanyaswa kimapenzi au kutengwa wakati wa utoto. Matokeo yake, wameendeleza hisia za kutokamilika na kujidharau wenyewe kwamba hawajakamilika.
Wazazi wao pia wanaweza kuwa waliwahi kuwa watumwa wa ngono na katika kuweka mlinganyo sawa wa tabia yao iliyokithiri, inawezekana waliwalea watoto wao bila maadili bora katika suala zima la mapenzi.
Mapenzi ya lazima mara nyingi huenda sambamba na na hisia za aibu, hatia na kutokuwa na thamani. Ingawa uzoefu wa mapenzi unaweza kuleta uhuru wa kitambo kifupi kutokana na hisia za aina hii, lakini bila kutegemea mhusika anaweza kujikuta akipambana na aibu, lawama na kujitweza mwenyewe. Watumwa wa ngono huwa hawana nguvu za kupambana na tabia zao.


Aina za Utumwa wa Ngono
Hizi dalili za athari zilizotokea kwa maisha ya mtumwa wa mapenzi:
Kumilikiwa - kila wakati kutafuta njia mpya za kukidhi kiu ya mapenzi. Wapo watu ambao kila siku wanabuni njia mpya ya kukidhi tamaa zake. Kama bosi, kwa mfano, amezoea kufanya mapenzi na sekretari wake au mfanya kazi wake, anaweza kuiendeleza tabia hiyo hata kufikia kutembea na wake wa wafanyakazi wake. Ngono ndicho kitu kinachokuwa kimemmiliki wakati wote.
Kulazimishwa - kuendelea kushiriki katika vitendo vya ngono hata kama vimemletea mhusika madhara na kukosa njia za kukoma tabia hiyo. Wapo watu ambao wamewahi kufumwa na wake au waume zao wakiwa na wafanyakazi wao wa ndani wakifanya mapenzi, lakini pamoja na aibu hiyo waliyoipata bado hawajakoma wanaendelea, na wazazi wengine hufikia hatua ya kutembea na binti zao au watoto wao wa kiume, hii hutokea katika baadhi ya watu ambao uraibu huu huwalazimisha kufanya vile hisia zao zinavyowatuma.
Kukata tamaa - kuona hatia au aibu katika uwezo wa kuidhibiti tabia ya ngono ya mhusika. Ili tabia hii ikome, ni lazima mhusika akiri kwamba ana tatizo hilo, lakini wengi wa waathirika huona aibu na hujisikia hatia, hasa kama walipatwa kufumaniwa na baadhi ya wanajamii wanaelewa vitendo vyao.


Kumaliza Utumwa wa Ngono
Hatua ya kwanza ya kumaliza tatizo la uraibu wa ngono, kama nilivyosema hapo juu, ni kulifahamu tatizo husika. Utakapogundua kwamba tabia yako haidhibitiki, ni wakati muafaka kwako kutafuta tatizo linalosababisha uraibu wako wa ngono. Matatizo haya yanaweza kuwa ya kifedha, kihisia na kimwili.
Ndiyo, wapo baadhi ya watu mara wanapokuwa na fedha wanataka kufanya mapenzi na mtu yeyote yule. Mwanaume mwenye fedha hupenda kutembea na wasichana wazuri wazuri na anaweza kufikia mahali akatembea hata na wake wa rafiki zake. Mbaya zaidi, anaweza kuwageukia hata wanafunzi kwa kuwarubuni kwa visenti vyake. Mwanamke mwenye fedha naye vile vile, anaweza kuwatafuta wanaume anaowataka na kuwahonga, ilimradi tu apate penzi.
Kama mtumwa wa ngono, kuna hatua zinazotakiwa kufuatwa ili kukusaidia kupambana na hisia zako za kutengwa kifikra. Kwa vile msongo wa mawazo wakati mwingine huchangia vitendo vya mapenzi ya lazima, mbinu za kupambana na msongo wa mawazo wakati mwingine husaidia.
Nchini Marekani kuna makundi kadhaa ambayo husaidia waathirika kupambana na madhara hayo. Taasisi hizo ni kama Sex & Love Addicts Anonymous, Sexaholics Anonymous & Sex Abusers Anonymous. Mhusika hata hivyo anaweza kupatiwa msaada na taasisi hizi kupitia mtandaoni au kwa kuwasiliana nao kwa simu.

No comments:

Post a Comment