Thursday, 24 October 2013
Matatizo gani yanatajwa sana kwenye ndoa za Watanzania? PATA JIBU.
Chris Mauki ambae ni mtaalamu wa Saikolojia pia ni Mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam, anakwambia katika kesi kubwa zinazoripotiwa kwa wingi na Wanandoa Tanzania sasa hivi, ni ndugu.
Anasema ‘Ishu ya nani anampa pesa baba wa mume, nani anampa pesa mama wa mke… ukipeleka pesa ukamwambia mume umemtumia baba laki tatu, kesho na yeye anapeleka milioni kwa baba yake alafu ukija kujua, kaeni pamoja muamue… kama mzazi wako akitaka pesa kwa nini afanye kwa siri? ukimsaidia mzazi bila kumwambia mwenza ikija kugundulika ndio tatizo… hii ishu inatajwa sana na Wanandoa wengi kuliko matatizo kama tabia za watoto, kazi n.k ‘
‘Mara nyingi Mwanamke anapoolewa na kuja kwenye ndoa anafikra kwamba Mama mkwe anaweza asinipende sasa ikitokea Mama Mkwe lada na dada za mume wakiongea kitu, tayari ni noma… anapokea vibaya kwa sababu tayari alikua na dhana hiyo’
Kwenye mstari mwingine, Mauki amesema ‘tatizo la pesa pia linazungumziwa sana.. na ishu ya pesa sio kwamba watu hawana pesa bali kinachozungumziwa ni matumizi ya hizo pesa, mmoja anamtuhumu mwenzake anatumia pesa ovyo bila mpangilio au kwenye matumizi ambayo hawakukubaliana, mfano pesa ya ujenzi mke anakwenda kununulia nguo na nywele, Wanaume wanalalamika kwamba mahitaji ya Wanawake yamekua makubwa kupitiliza’
‘Wanaume wanaweza kupanga kabla ya kupata pesa kwamba akiipata atafanya kitu hiki na hiki lakini Mwanamke anaweza kuplan kuhusu matumizi ya pesa kabla hata ya kuipata, anaweza kupata pesa kesho alafu akaitumia kwenye vitu vingine alafu asiguse hata kimoja ambacho kilikua kwenye mpango, vilevile Mwanamke anaweza ku-negotiate wakati hana hata pesa wakati huo’ – Mauki
‘Mwanamke ni ngumu sana akisema anakwenda Kariakoo kununua kitu flani alafu akaja na kitu hichohicho, utakuta kaongeza hiki na kile wakati Mwanaume akitoka kwenda kununua shati ni rahisi kurudi nalo peke yake bila kuongeza kitu, hii ni ishu ya kuelewa na kufahamu kwamba Wanawake ni watu wa aina gani manake mwisho wa siku bila kuelewana mtagombana kila siku’ -Mauki
Matatizo mengine yanayotajwa ni pamoja na watu kutoka nje ya ndoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment