ELIMU KWANZA

ELIMU KWANZA
KWETU FEDHA SIO KIPAUMBELE.

Sunday 17 November 2013

MIAKA HATARI YA KUVUNJIKA KWA NDOA


Watafiti wa masuala ya uhusiano na ndoa wana kalenda za miaka ya hatari iliyotafsiriwa sambamba na sababu zinazoweza kuvuruga uhusiano na kuwafanya watu waliokuwa wakipendana kuachana.

Hivyo kwa dondoo tu nimeona ni vyema niwafundishe watu wanaoishi kwenye ndoa sababu zinazotafsiri ukomo wa mapenzi yao kulingana na miaka husika iliyotafsiliwa na watalaamu wa masuala ya ndoa na uhusiano.

eti,,WAPENZI WAKUTANE KIMWILI MARA NGAPI KWA WIKI, WATOSHEKE?


Kwa wiki nzima nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki tendo la ndoa na kulidhika.

Wengi kati ya hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili watosheke?

Jibu la swali hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini? Katika hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini, hii ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu.
www.mahabaleo.blogspot.com

Thursday 14 November 2013

Fahamu sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati!


HII ni safu ya wale walio tayari kuambiwa ukweli hata kama utawauma. Ndiyo...siku zote ukweli huwa unauma. Karibuni sana marafiki katika uwanja wetu ili tuweze kupanuana mawazo katika mambo ya uhusiano.
Kabla sijaenda moja kwa moja katika mada yenyewe, nawakumbusha kwamba kitabu changu cha Let’s Talk About Love sasa kinapatikana mitaani, utasoma mada mbalimbali za mapenzi pamoja na Love Messages kali zitakazompagawisha mpenzi wako. Usikose nakala yako.

Friday 8 November 2013

Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha-9

Tunaendelea na mada yetu ya Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha kutoka pale tulipoiishia wiki iliyopita.
Endelea...
Nilishaeleza huko nyuma kwamba ni vizuri kuzungumza wakati wa tendo. Hata kama wewe ni mvivu, jibidishe katika kuulainisha ulimi wako ili uwe unatamka maneno matamu, yanayoongeza hamu na mzuka wa kuendelea kuwajibika shughulini.

Wednesday 6 November 2013

Faida 4 za kuwa na wivu kwa mumeo

ASSALAM Alaikum! Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi kupitia safu hii ya Mashamsham nikiamini muwazima na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.
Mpenzi msomaji wangu, utakumbuka wiki iliyopita nilizungumzia sababu za baadhi ya wake za watu kutembea na wapangaji wao au wenye nyumba. Ni mada iliyoonekana kuwavutia wengi, nadhani ni kwa sababu ni tabia inayoonekana kushamiri sana mtaani.

Sunday 3 November 2013

KWA PENDA PENDA;WEWE MSICHANA / MWANAMKE UNAKERWA NA KUTONGOZWA OVYO NA WANAUME ?. DAWA YAKE HII HAPA.


Leo nimeona nizungumze juu ya tabia ya baadhi ya wanawake kutongozwa hovyo. Kiukweli ni tabia ambayo inakera. Kila ukipita huku unaitwa, ukienda kule unaitwa, hili tatizo lipo kwa wanawake wengi hasa wa mijini.

Kiukweli hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunapoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwatomasa tomasa sehemu zao nyeti bila ridhaa yao. Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao.