ELIMU KWANZA

ELIMU KWANZA
KWETU FEDHA SIO KIPAUMBELE.

Wednesday, 30 October 2013

yajuwe MAMBO MANNE YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA!

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia. Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha sana!

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia.

Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Monday, 28 October 2013

MADHARA YA KITAALAMU YA KUWA NA WAPENZI WENGI!!!Usipuuzie soma hapa....

KILA kinachotokea leo katika maisha yako ni matokeo ya namna ulivyowaza na kutenda kipindi cha nyuma. Maisha ni mipango.
Hata katika uhusiano na mapenzi ni hivyohivyo. Kama hutakuwa mkweli, hutaishi maisha safi na utaonesha picha mbaya kwa jamii, kesho utakutana na majibu yake.


Umakini katika maisha ya uhusiano ni mzuri, kwanza kutakujenga kiakili, moyo hautakuwa na ukakasi maana una msimamo thabiti. Suala la kupenda ni muhimu.
Unaweza kupendwa lakini usipende. Unaweza kuwa na mwenzi wako ambaye mmefunga ndoa kabisa, lakini usiwe na mapenzi naye au pendo likapungua na baadaye kuyeyuka kabisa.
Hifadhi pendo moyoni mwako. Penzi ni uwekezaji. Lazima uwekeze pendo moyoni mwako, ujifunze kuwa katika uhusiano sahihi ili siku zijazo uyafurihie maisha.
Mapenzi hayatakuwa na maana kwako kama huna uwezo wa kupenda. Faragha haitakuwa na maana kwako kama hutakuwa na hamu na tendo lenyewe. Wengi wana tatizo hili lakini hawajajua namna ya kujitibu.

MAPENZI;Fedha, uzuri si kinga ya mapenzi, kuna hiki kitu cha ziada hapa!!!!


WAKATI akili yangu ikianza kupata ufahamu, nilikuwa natatizika na kuwaza kitu gani hasa katika mapenzi kinaweza kumfanya mtu atulie ndani ya penzi lake. Niliamini kuwa na fedha ndiyo dawa ya mtu kumtuliza mpenzi wake au kwa mwanamke kuwa mzuri na mwenye sifa zote, ndiyo dawa ya kumfanya mpenzi wako atulie.
Baada ya kukua na kuingia katika dunia ya ufahamu wenye mitihani mingi ya mapenzi, nimegundua kuna utofauti mkubwa katika vitu nilivyoviwaza.
Wakati nakua, nilikutana na matukio ambayo niliona kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, lakini baada ya kupevuka, nilipata majibu ya maswali yaliyonisumbua kipindi kile cha utoto.
Sikuamini mke wa tajiri kufanya mapenzi na muuza mchicha, mwanaume mwenye mke mzuri kutembea na changudoa au msichana wa kazi asiyejua kuvaa wala kuoga.
Baada ya kuingia katika kazi hii ya kukumbushana mambo ya mapenzi, nilipata maswali mawili ya watu wawili tofauti lakini yalikuwa na jibu moja.

Thursday, 24 October 2013

Matatizo gani yanatajwa sana kwenye ndoa za Watanzania? PATA JIBU.




Chris Mauki ambae ni mtaalamu wa Saikolojia pia ni Mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam, anakwambia katika kesi kubwa zinazoripotiwa kwa wingi na Wanandoa Tanzania sasa hivi, ni ndugu.

Anasema ‘Ishu ya nani anampa pesa baba wa mume, nani anampa pesa mama wa mke… ukipeleka pesa ukamwambia mume umemtumia baba laki tatu, kesho na yeye anapeleka milioni kwa baba yake alafu ukija kujua, kaeni pamoja muamue… kama mzazi wako akitaka pesa kwa nini afanye kwa siri? ukimsaidia mzazi bila kumwambia mwenza ikija kugundulika ndio tatizo… hii ishu inatajwa sana na Wanandoa wengi kuliko matatizo kama tabia za watoto, kazi n.k ‘

Wednesday, 23 October 2013

JUA VITU VINAVYOWAHARIBIA WANAWAKE KIMAPENZI




KUNA msemo kuwa: “Wanawake, mwalimu wao ni kipofu.” Mimi siuamini kwa maana umekaa kiukandamizaji zaidi. Haujengi heshima kwa mtu wa jinsi ya kike tangu analizaliwa mpaka anapoingia kaburini. Binafsi naamini wapo wenye uelewa mkubwa lakini wanashambuliwa na mapokeo ya samaki mmoja akioza.

Ni msemo ambao ukiingia kwenye vichwa vya watu unaweza kuwafanya wanaume wawadharau hata mama zao. Mama anatoa mafundisho lakini kijana anasikiliza, linaingilia sikio la kwanza na kutokea la pili. Kichwani anajiongeza: “Aah, hawa si mwalimu wao kipofu?”

FAHAMU Hatua 10 za Kuchagua Mchumba




Kwanza niwasalimu wasomaji na wafuatiliaji wa blog hii www.mahabaleoo.blogspot.com ambayo inaendelea kujitahidi katika kuelimisha na hata kukutabainisha mambo jinsi yalivyo sambamba na kukujuza ambavyo huyafahamu.
Kwa siku ya leo jumatano nimependa niwaandalie jinsi yakumtambua mchumba mwema wa kuoa.

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Monday, 21 October 2013

ZIFAHAMU FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI


Kiafya

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu

JUA,Namna ya Kufanya Mapenzi Kipindi Cha Ujauzito


Habari za jioni wapenzi wasomaji wangu! Katika mfululizo wa kusasambua leo naomba niongelee kuhusu kufanya mapenzi kipindi cha ujauzito! Nimefikia hatua mara baada ya mabishano na mijadala kadhaa ya watu wazima kuhusu mapenzi, staili na madhara kipindi cha ujauzito! kwa leo mimi ntasema machache nnaimani mengi yanajulikana tayari.

Fahamu matumizi na maana ya rangi za shanga zinazovaliwa kiunoni na wanawake kwenye sita kwa sita na Rangi zake






NI KWAMUJIBU WA FLOCLAASSIC.COM

Mpenzi msomaji wa blog hii,naomba tuongelee rangi za shanga kwa wale wanaopenda kuvaa shanga.
Najua wengi mtakuwa mnafahamu rangi na maana zake lakini kwa wale wasiojuwa ama wanaopenda kuvaa lakini wanajinunulia rangi yeyote huu ndo wakati mwafaka.

Wanaume wengi wanaopenda wanawake wao wavae shanga ili kusisimuana tu .Je mnafahamu zinamaanisha nini?....Karibu tujifunze pamoja.

Katika swala la mahaba shanga hutumika kusisimuana haswa pale utakapompata mwanaume anayejuwa kuzitumia vizuri na unaweza kuvaa hata kumi ukitaka .
Jana niliguswa sana na simulizi la rafiki yangu juu ya shanga, hivyo nikaona boraniandike na wengne wajue.Hii ni sehem ndgo ya simulizi lake.

ZIJUWE, sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati!


HII ni safu ya wale walio tayari kuambiwa ukweli hata kama utawauma. Ndiyo...siku zote ukweli huwa unauma. Karibuni sana marafiki katika uwanja wetu ili tuweze kupanuana mawazo katika mambo ya uhusiano.
Haya sasa twende kwenye mada yetu. Nazungumzia sifa za mwanaume ambaye ana mapenzi ya kweli. Ni mada ambayo unaweza kuiona ya kawaida sana lakini ndani yake kuna mbinu madhubuti zitakazokufanya ugundue kuwa upo kwenye uhusiano wa kweli au wa longolongo!