ELIMU KWANZA

ELIMU KWANZA
KWETU FEDHA SIO KIPAUMBELE.

Saturday, 21 December 2013

MPE MPENZI WAKO SABABU YA KUWA NA WEWE!!!SOMA HAPA KUJUA NAZUNGUMZIA NINI.....

KARIBUNI kwenye uwanja wetu tujadiliane kuhusu mapenzi. Marafiki zangu, katika uhusiano umakini wa hali ya juu huhitajika ili uweze kuwa bora kila siku na kuufanya uhusiano wako kuwa wenye nguvu na usiotetereka! Katika hili hutegemea zaidi jinsi unavyoendesha uhusiano wako.

Ukitaka mpenzi wako akuchoke au umchoke, wewe ndiye mwamuzi, lakini pia ukitaka mpenzi asikuchoke au usimchoke wewe ndiye mwenye uamuzi kwa kuwa una uwezo wa kuyafanya yote hayo. Hebu nikuulize, umempa sababu mwenzako ya kuwa na wewe?

Saturday, 14 December 2013

MAMBO YATAKAYOKUFANYA UONEKANE BORA KWA MPENZI!

NDUGU zangu, kuna ambao wapo katika uhusiano lakini hawajui mambo ya kufanya ili wawe bora kwa wapenzi wao. Mada hii itagusia pande mbili. Upande wa kwanza ni kwa wale ambao ndiyo kwanza wapo katika hatua za mwanzo kabisa na wapenzi wao na upande wa pili ni kwa wale ambao tayari wapo katika uhusiano lakini hawajui jinsi ya kuwafanya wawe bora kwa wapenzi wao.




Inawezekana wewe ukawa mmoja wao, sasa huna sababu ya kukata tamaa na kuona kuwa huna thamani tena kwa mpenzi wako. Kwa kufuatilia vyema vipengele vifuatavyo, naamini kwa namna moja au nyingine utakuwa mpya na penzi lako litazidi kudumu zaidi na zaidi.


MWANZO WA PENZI


Sunday, 17 November 2013

MIAKA HATARI YA KUVUNJIKA KWA NDOA


Watafiti wa masuala ya uhusiano na ndoa wana kalenda za miaka ya hatari iliyotafsiriwa sambamba na sababu zinazoweza kuvuruga uhusiano na kuwafanya watu waliokuwa wakipendana kuachana.

Hivyo kwa dondoo tu nimeona ni vyema niwafundishe watu wanaoishi kwenye ndoa sababu zinazotafsiri ukomo wa mapenzi yao kulingana na miaka husika iliyotafsiliwa na watalaamu wa masuala ya ndoa na uhusiano.

eti,,WAPENZI WAKUTANE KIMWILI MARA NGAPI KWA WIKI, WATOSHEKE?


Kwa wiki nzima nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki tendo la ndoa na kulidhika.

Wengi kati ya hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili watosheke?

Jibu la swali hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini? Katika hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini, hii ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu.
www.mahabaleo.blogspot.com

Thursday, 14 November 2013

Fahamu sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati!


HII ni safu ya wale walio tayari kuambiwa ukweli hata kama utawauma. Ndiyo...siku zote ukweli huwa unauma. Karibuni sana marafiki katika uwanja wetu ili tuweze kupanuana mawazo katika mambo ya uhusiano.
Kabla sijaenda moja kwa moja katika mada yenyewe, nawakumbusha kwamba kitabu changu cha Let’s Talk About Love sasa kinapatikana mitaani, utasoma mada mbalimbali za mapenzi pamoja na Love Messages kali zitakazompagawisha mpenzi wako. Usikose nakala yako.

Friday, 8 November 2013

Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha-9

Tunaendelea na mada yetu ya Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha kutoka pale tulipoiishia wiki iliyopita.
Endelea...
Nilishaeleza huko nyuma kwamba ni vizuri kuzungumza wakati wa tendo. Hata kama wewe ni mvivu, jibidishe katika kuulainisha ulimi wako ili uwe unatamka maneno matamu, yanayoongeza hamu na mzuka wa kuendelea kuwajibika shughulini.

Wednesday, 6 November 2013

Faida 4 za kuwa na wivu kwa mumeo

ASSALAM Alaikum! Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi kupitia safu hii ya Mashamsham nikiamini muwazima na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.
Mpenzi msomaji wangu, utakumbuka wiki iliyopita nilizungumzia sababu za baadhi ya wake za watu kutembea na wapangaji wao au wenye nyumba. Ni mada iliyoonekana kuwavutia wengi, nadhani ni kwa sababu ni tabia inayoonekana kushamiri sana mtaani.

Sunday, 3 November 2013

KWA PENDA PENDA;WEWE MSICHANA / MWANAMKE UNAKERWA NA KUTONGOZWA OVYO NA WANAUME ?. DAWA YAKE HII HAPA.


Leo nimeona nizungumze juu ya tabia ya baadhi ya wanawake kutongozwa hovyo. Kiukweli ni tabia ambayo inakera. Kila ukipita huku unaitwa, ukienda kule unaitwa, hili tatizo lipo kwa wanawake wengi hasa wa mijini.

Kiukweli hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunapoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwatomasa tomasa sehemu zao nyeti bila ridhaa yao. Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao.

Wednesday, 30 October 2013

yajuwe MAMBO MANNE YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA!

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia. Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha sana!

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia.

Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Monday, 28 October 2013

MADHARA YA KITAALAMU YA KUWA NA WAPENZI WENGI!!!Usipuuzie soma hapa....

KILA kinachotokea leo katika maisha yako ni matokeo ya namna ulivyowaza na kutenda kipindi cha nyuma. Maisha ni mipango.
Hata katika uhusiano na mapenzi ni hivyohivyo. Kama hutakuwa mkweli, hutaishi maisha safi na utaonesha picha mbaya kwa jamii, kesho utakutana na majibu yake.


Umakini katika maisha ya uhusiano ni mzuri, kwanza kutakujenga kiakili, moyo hautakuwa na ukakasi maana una msimamo thabiti. Suala la kupenda ni muhimu.
Unaweza kupendwa lakini usipende. Unaweza kuwa na mwenzi wako ambaye mmefunga ndoa kabisa, lakini usiwe na mapenzi naye au pendo likapungua na baadaye kuyeyuka kabisa.
Hifadhi pendo moyoni mwako. Penzi ni uwekezaji. Lazima uwekeze pendo moyoni mwako, ujifunze kuwa katika uhusiano sahihi ili siku zijazo uyafurihie maisha.
Mapenzi hayatakuwa na maana kwako kama huna uwezo wa kupenda. Faragha haitakuwa na maana kwako kama hutakuwa na hamu na tendo lenyewe. Wengi wana tatizo hili lakini hawajajua namna ya kujitibu.

MAPENZI;Fedha, uzuri si kinga ya mapenzi, kuna hiki kitu cha ziada hapa!!!!


WAKATI akili yangu ikianza kupata ufahamu, nilikuwa natatizika na kuwaza kitu gani hasa katika mapenzi kinaweza kumfanya mtu atulie ndani ya penzi lake. Niliamini kuwa na fedha ndiyo dawa ya mtu kumtuliza mpenzi wake au kwa mwanamke kuwa mzuri na mwenye sifa zote, ndiyo dawa ya kumfanya mpenzi wako atulie.
Baada ya kukua na kuingia katika dunia ya ufahamu wenye mitihani mingi ya mapenzi, nimegundua kuna utofauti mkubwa katika vitu nilivyoviwaza.
Wakati nakua, nilikutana na matukio ambayo niliona kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, lakini baada ya kupevuka, nilipata majibu ya maswali yaliyonisumbua kipindi kile cha utoto.
Sikuamini mke wa tajiri kufanya mapenzi na muuza mchicha, mwanaume mwenye mke mzuri kutembea na changudoa au msichana wa kazi asiyejua kuvaa wala kuoga.
Baada ya kuingia katika kazi hii ya kukumbushana mambo ya mapenzi, nilipata maswali mawili ya watu wawili tofauti lakini yalikuwa na jibu moja.

Thursday, 24 October 2013

Matatizo gani yanatajwa sana kwenye ndoa za Watanzania? PATA JIBU.




Chris Mauki ambae ni mtaalamu wa Saikolojia pia ni Mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam, anakwambia katika kesi kubwa zinazoripotiwa kwa wingi na Wanandoa Tanzania sasa hivi, ni ndugu.

Anasema ‘Ishu ya nani anampa pesa baba wa mume, nani anampa pesa mama wa mke… ukipeleka pesa ukamwambia mume umemtumia baba laki tatu, kesho na yeye anapeleka milioni kwa baba yake alafu ukija kujua, kaeni pamoja muamue… kama mzazi wako akitaka pesa kwa nini afanye kwa siri? ukimsaidia mzazi bila kumwambia mwenza ikija kugundulika ndio tatizo… hii ishu inatajwa sana na Wanandoa wengi kuliko matatizo kama tabia za watoto, kazi n.k ‘

Wednesday, 23 October 2013

JUA VITU VINAVYOWAHARIBIA WANAWAKE KIMAPENZI




KUNA msemo kuwa: “Wanawake, mwalimu wao ni kipofu.” Mimi siuamini kwa maana umekaa kiukandamizaji zaidi. Haujengi heshima kwa mtu wa jinsi ya kike tangu analizaliwa mpaka anapoingia kaburini. Binafsi naamini wapo wenye uelewa mkubwa lakini wanashambuliwa na mapokeo ya samaki mmoja akioza.

Ni msemo ambao ukiingia kwenye vichwa vya watu unaweza kuwafanya wanaume wawadharau hata mama zao. Mama anatoa mafundisho lakini kijana anasikiliza, linaingilia sikio la kwanza na kutokea la pili. Kichwani anajiongeza: “Aah, hawa si mwalimu wao kipofu?”

FAHAMU Hatua 10 za Kuchagua Mchumba




Kwanza niwasalimu wasomaji na wafuatiliaji wa blog hii www.mahabaleoo.blogspot.com ambayo inaendelea kujitahidi katika kuelimisha na hata kukutabainisha mambo jinsi yalivyo sambamba na kukujuza ambavyo huyafahamu.
Kwa siku ya leo jumatano nimependa niwaandalie jinsi yakumtambua mchumba mwema wa kuoa.

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Monday, 21 October 2013

ZIFAHAMU FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI


Kiafya

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu

JUA,Namna ya Kufanya Mapenzi Kipindi Cha Ujauzito


Habari za jioni wapenzi wasomaji wangu! Katika mfululizo wa kusasambua leo naomba niongelee kuhusu kufanya mapenzi kipindi cha ujauzito! Nimefikia hatua mara baada ya mabishano na mijadala kadhaa ya watu wazima kuhusu mapenzi, staili na madhara kipindi cha ujauzito! kwa leo mimi ntasema machache nnaimani mengi yanajulikana tayari.

Fahamu matumizi na maana ya rangi za shanga zinazovaliwa kiunoni na wanawake kwenye sita kwa sita na Rangi zake






NI KWAMUJIBU WA FLOCLAASSIC.COM

Mpenzi msomaji wa blog hii,naomba tuongelee rangi za shanga kwa wale wanaopenda kuvaa shanga.
Najua wengi mtakuwa mnafahamu rangi na maana zake lakini kwa wale wasiojuwa ama wanaopenda kuvaa lakini wanajinunulia rangi yeyote huu ndo wakati mwafaka.

Wanaume wengi wanaopenda wanawake wao wavae shanga ili kusisimuana tu .Je mnafahamu zinamaanisha nini?....Karibu tujifunze pamoja.

Katika swala la mahaba shanga hutumika kusisimuana haswa pale utakapompata mwanaume anayejuwa kuzitumia vizuri na unaweza kuvaa hata kumi ukitaka .
Jana niliguswa sana na simulizi la rafiki yangu juu ya shanga, hivyo nikaona boraniandike na wengne wajue.Hii ni sehem ndgo ya simulizi lake.

ZIJUWE, sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati!


HII ni safu ya wale walio tayari kuambiwa ukweli hata kama utawauma. Ndiyo...siku zote ukweli huwa unauma. Karibuni sana marafiki katika uwanja wetu ili tuweze kupanuana mawazo katika mambo ya uhusiano.
Haya sasa twende kwenye mada yetu. Nazungumzia sifa za mwanaume ambaye ana mapenzi ya kweli. Ni mada ambayo unaweza kuiona ya kawaida sana lakini ndani yake kuna mbinu madhubuti zitakazokufanya ugundue kuwa upo kwenye uhusiano wa kweli au wa longolongo!

Friday, 18 October 2013

TIBA ASILIA YA KUACHA KUPIGA PUNYETO

Punyeto ( kwa wanaume ) ni kitendo cha mwanaume, kujifikisha mwenyewe kileleni kwa kujichua uume hadi kumwaga mbegu za kiume. Uchunguzi unaonyesha katika watu wa jinsia ya kiume kumi wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 45, angalau wanne kati yao wamewahi kupiga punyeto katika kipindi fulani cha maisha yao, na wawili kati yao wanajihusisha na upigaji punyeto. Uzoefu unaonyesha, asilimia kubwa ya wanaume wanao piga punyeto huanza katika umri wa kubalehe ( miaka 14-16 ), wengine huachana na tabia hiyo mara baada ya kupata wapenzi wa kike ama kuoa na wengine huendelea na tabia hiyo hata baada ya kuoa .

HAYA HAPA MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA UPENDO KATIKA MAPENZI




katika Mapenzi kuna vitu vingi unaweza kumfanyia Mpenzi wako ukamfurahisha na kumfanya azidishe Mapenzi ila katika safu hii nitazungumzia Mambo machache muhimu yatakayokusaidia kuboresha na kudumisha penzi lako kwa umpendaeKARIBU:

YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA UPENDO:

1.KUMNUNULIA ZAWADI MPENZI WAKO:
» Zawadi ni moja ya sehemu husika katika Mapenzi inayoweza kufanya penzi likawa bora na lenye kupendeza siku zote, faham kwamba hakuna mtu asiependa kupewa zawadi na kila anaepewa zawadi siku zote hujihisi kama ni mtu anaependwa na anaejaliwa na kuthaminiwa hususani katika ulimwengu wa Mapenzi unapompa mpenzi wako zawadi basi faham ya kwamba utamfanya mpenzi wako ajione kama ni wapekee kwako na anathamani kubwa kwako hivyo hatosita kudhihirisha mapenzi yake kwako, kikubwa zingatia pindi unaponunua zawadi kwa ajili ya kumpa mpenzi wako jitahidi kuwa mbunifu na uwe ni mwenye kubadilika sio kila siku zawadi zile zile zinajirudia kwa kufanya hivi utamboa mpenzi wako kuwa mbunifu na jaribu kumpa mpenzi wako zawadi zenye kutunzika mfano kama Card, maua, nguo n.k. Utamfanya azidi kukupenda zaidi na zaidi.

2. MSIFIE MPENZI WAKO:

FAHAMU, NAMNA YA KUMVUTIA MTU YEYOTE YULE ALIYEUTEKA MOYO WAKO!


HISIA za mapenzi hutokea ndani kabisa ya moyo. Kila mmoja ana uhuru na haki ya kupenda. Huwezi kuchaguliwa wa kumpenda! Mapenzi ni maisha ya mtu katika uhalisia wake.
Maana yake ni kwamba, kama utakuwa na mtu ambaye moyo wako hauna mapendo ya dhati kwake, tafsiri yake ni kwamba, maisha yako yote yatakuwa yenye mateso kila siku.

Utalala na mtu usiyempenda, utaamka naye na utaambatana naye baadhi ya sehemu wakati moyo wako haukuwa tayari kuwa naye. Hilo ni tatizo. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya wazazi bado wana mawazo na fikra za kizamani.

Thursday, 17 October 2013

YA FAHAMU MADHARA YA KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE.

Leo tunageuza shilingi upande wa pili kuelezea madhara ya kuruka ukuta (kufanya ngono kinyume cha maumbile), baada ya kuona madhara ya wanawake kurukwa na nini kifanyike.
Wanaume wengi walinilaumu na kuniona sitendi haki kwa kuwaelezea wanawake tu wakati mchezo huwa una athari kwa mtenda na mtendewa.
Kama nilivyoelezea kwenye mada za wiki kadhaa zilizopita, mchezo huu unatumika sana katika mapenzi ya sasa, watoto wa mjini wana usemi wao kwa kitu kilichovuma kuwa ‘ndiyo habari ya mjini’.
Mchezo huu umekuwa ukipendwa sana na wanaume wengi ambao wengi wao huwa hawatumii kinga na kusababisha wengi kupata magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Lakini mchezo wa kuruka ukuta umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanaume wanaoufanya kwa muda mrefu.

MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAUME HUITAJI KUTOKA KWA MKEWE



NI matumaini yangu kuwa umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida. Wiki iliyopita utakumbuka niliishia kuzungumzia suala la busara. Nikasema mwanamke anaweza kuwa chanzo cha furaha kwa mumewe endapo atatumia busara kwa kiwango kinachotakiwa.

Kwa kifupi wanaume wanahitaji sana busara ya mwanamke na kama mwanamke ukiweza kuwa na busara katika kumtatulia matatizo yake hata kwa kumpa mawazo yako na kumpa moyo, ataona umuhimu wako na wakati mwingine kukushirikisha kila afanyalo kabla ya kulifanya hasa baada ya kuona anaishi na mwanamke mwenye busara.

Tuesday, 15 October 2013

UJUWE UTUMWA WA NGONO


WATU wengi ni watumwa wa ngono bila wenyewe kujua. Lakini ubongo una kazi gani katika utumwa wa ngono? Ni njia gani zilizopo katika kupambana na uraibu na kurejea katika hali ya kawaida pamoja na kujizatiti na kujihakikishia tena kuwa na maisha ya mapenzi yaliyo bora? Kitu kilicho bora, ninaamini ni kwenda hatua kwa hatua katika kulielezea tatizo hili.

Saturday, 12 October 2013

NI WAKATI WA UKOMBOZI KWA BARA LA AFIKA,HOTU HIYO KUTOLEWA NA MWANAHARAKATI OSCAR SAMBA.

FANYA HAYA KUMFANYA MWANAMKE AKUPENDE NA UMVUTIE DAIMA!!!!!

 
Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote. 
Hapa kuna njia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ; 
1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.
2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia. 

ZIJUE FAIDA ZA KUMSIFIA MUPENZI WAKO


YAPO mengi mazuri ambayo huenda mpenzi wako aliwahi kukufanyia, je uliwahi kumshukuru kwa kukufanya ufarijike? Naamini Mungu amekujaalia kuwa na mpenzi mzuri, mwenye kila sifa ambayo ulitamani awe nayo, je ulishawahi kumsifia hata kwa kumwambia ni mzuri?
Huenda ulishawahi kufanya hivyo lakini kwa taarifa yako wapo ambao wanahisi kufanya hivyo eti ni ulimbukeni. Ulimbukeni? Kumsifia mpenzi wako unaona ni ulimbukeni wakati wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, wanawake ni watu wanaopenda kusifiwa sana hata kwa madogo wanayoyafanya?
Unaona hatari gani kumsifia mpenzi wako kuwa ni mzuri? Unadhani unatumia nguvu gani kumsifia mpenzi wako kutokana na

Friday, 4 October 2013

VYAKULA VINAVYO ONGEZA NGUVU ZA KIUME.


Kuna Aina 2 Ya Vyakula Ambavyo Vimefanyiwa Utafiti Na Kubaini Kuwa Ni Moja Ya Vyakula Vinavyosaidia Kuongeza Nguvu Za Kiume Na Havina Madhara Katika Engezeko La Nguvu Za Kiume, Katika Vyakula Hivyo Vyenye Uwezo Wa Kuongeza Nguvu Za Kiume Kiasili Ni:

1. TANGAWIZI
- Tangawizi Ni Moja Ya Chakula Kinachoweza Kurejesha Nguvu Za Kiume, Unaweza Kuichemsha Tangawizi Na Ukatumia Kwa Kuinywa Kama Chai Asubuhi, Mchana Na Jioni Pia Tangawizi Unaweza Ukaitumia Katika Mchanganyiko Wa Kiasili Kwa Kutumia Habat Soda,Asali,Kitunguu Saumu Na Tangawizi Yenyewe.


JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU:
Chukua Tangawizi Na Kitunguu Saumu Vitwange Kisha Vichanganye Na Asali Pamoja Na Unga Wa Habat Soda Na Uwe Unakunywa Mchanganyiko Huu Kwa Kutumia Kijiko Cha Chai Kimoja Kutwa Mara 3 Kwa Muda Wa Wiki Moja Na Utaona Mabadiliko.

2. TIKITI MAJI:
-Chakula Kingine Kinachosaidia Katika Upande Wa Kuongeza Nguvu Za Kiume Ni Tunda La Tikiti Maji, Unaweza Ukachukua Tikiti Lako Ukalikata Na Kutengeneza Juice Ya Tikiti Kisha Unakunywa Ila Sio Lazima Utengeneze Juice Hata Lenyewe Tu Unaweza Ukalila. Ila Jitahidi Kutumia Tunda Hili Hata Kila Siku Kwani Linasaidia Sana Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu Za Kiume

Thursday, 3 October 2013

MAHUSIANO NA AFYAJUA NAMNA YA KUONGEZA MVUTO WA KIMAPENZI



NA LILIANI SETH
Mahusiano na afya kwa hakika vinashabiana kwani vinategemeana kwa kufanya kuwepo furaha angalau kidogo kwa mwanadamu ni wazi kama hauna mahusiano ya aina yeyote ni dhahiri afya yako itadhorota hivyo tarajia afya njema kama unamahusiano.Mahusiano ni neno pana kulingana na uzito na ugumu wa kuzingatia katika mahusiano na pia yapo mahusiano ya aina mbalimbali kama kati ya wazazi na watoto wao,familia moja na nyingine,mtu na mtu na hata shirika na shirika lakini leo nitazungumzia mahusiano ya mtu na mtu
Ni rahisi kujenga mahusiano na mtu yeyote lakini ni vigumu kudumisha na kufurahia mahusiano hayo kutokana na utofauti kama wa rika,hali ya kimaisha,tabia,imani na mengineyo mengi hivyo ni vizuri kabla ya kuanzisha mahusiano ni lazima ukubali kuzingatia vitu Fulani ili kuhakikisha unapokuwa na mahusiano yanadumu kwa wakati wote.Katika maisha tunayoishi tunategemea mahusiano ili kutoa na kupokea vitu Fulani ambavyo inawezekana vinafaida au havina faida kwa wakati mwingine vinadhoofu miili yetu

Mojawapo ya ishara ya afya njema ni furaha japo kwa wakati mwingine mtu anaweza kuwa na furaha ya usoni na wala si moyoni
JINSI YAKUTENGENEZA FURAHA YA KWELI
-Kuikubali imani yako[dini]kuwa na imani ambayo itakuongoza kutekeleza mema
-kula lishe bora[balance diet]
-Fanya vitu unavyofurahia[hoby kama kuogelea,kucheza,kuimba n.k
-Kuwa zaidi ya usafi[nadhifu na wakupendeza]
-Jikubali kabla ya mwingine kuonyesha kukubali[usitamani kuwa na maumbile ambayo ni wazi hutoweza kuwa nayo kama ufupi,urefu n.k]
-Kubali kusamehe wengine
-Fanya shughuli zako za kimaisha kwa bidii[ikiwa ni kazini,shule na hata nyumbani]
-Jisikie kuwajali,kuwapenda,kuwathamini na hata kuwasaidia wengine
Ni dhahiri furaha ya kweli haihitaji ubinafsi ni lazima kuwepo sababu ya mwingine kuongeza furaha yako japo kama kwa mazingira Fulani inawezekana kutokuwepo mtu wa kuongeza furaha yako kwa kuona hivyo unawajibu wa kuzingatia zaidi niliyoyazungumzia hapo juu ili kuhakikisha unaendelea kuwa na afya njema
Mahusiano ya mtu na mtu inawezekana yakawa ya mwanaume na mwanamke[msichana na mvulana na hata jinsia moja]
Japo watu wengi hawajali na wala kuumizwa na mahusiano ya jinsia moja na hii ni kwasababu mahusiano ya jinsia tofauti yanalenga uhitaji zaidi kwa kutoa na kupokea kitu zaidi ya kawaida,neno kawaida ni hali ya mazoea na mtu wa aina yeyote wala uzingatiaji wa kitu chochote hauhitajiki
Kama upo uhusiano wa jinsia tofauti ni wazi kipo kitu zaidi ya kawaida na ni lazima vipo vitu vya kuzingatia ili isije ikawa ni kawaida.Mahusiano yanahitaji vitu vitatu[3]pekee
-Akili
-Moyo
-Mwili
Na kwa hakika vinatakiwa kulingana na wala siyo kingine kuzidi kwa mwenzake kwani kwa kuzingatia hivyo tunaweza kuhifadhi furaha ya kweli,Akili ni uwezo wa kufikiri na kupambanua jambo na moyo ni uhifadhi kwa yaliyo mazuri na hata mabaya lakini mwili ni ukubali wa viungo vya nje na ndani ya mwili kufanya kazi hivyo ili kuwepo kwa afya njema hutegemea utendaji mzuri wa akili,moyo na mwili na
Vyote hivyo vipo ndani maamuzi yetu kwa ruksa ya mwenyezi mungu pekee hivyo tunawajibu wa kuvitumia tunavyotaka lakini matokeo ni jibu la utumiaji mzuri au mbaya vitu hivi.jiulize ni kwanini unapokea maumivu katika mahusiano ikiwa umepewa uwezo wa kutawala vitu hivi vitatu inawezekana ni uzembe wakutozingazia ulinganifu wa vitu hivi.
Ni wazi kila mmoja anatamani kuongeza furaha kwa kuwa katika mahusiano kwa kupitia blog hii inawezekana kuamua kupata mahusiano sahihi na yatakayokidhi malengo yako
NAMNA YA KUTUMIA AKILI,MOYO NA MWILI KATIKA MAHUSIANO
-AKILI katika mahusiano inatumika katika kufikiri kwamba Yule unayetamani kuwa na mahusiano naye mnashabiana kitabia,rika,hali ya maisha na mengineyo japo mengine hayana umuhumu kwa kuzingatia makubaliano ya wanamahusiano
-Moyo ni sehemu ya mahusiano kwa kupitia mbinu mbalimbali unaweza kutambua nguvu ya hisia ulizonazo kwa unayemkusudia kuwa na mahusiano naye
-mwili pia huwakilisha na kutimiza yatakayo moyo hivyo ni lazima ukubali vitu hivi kufanya kazi pamoja bila upendeleo ili kupata kitu timamu
Mahusiano ni jambo la hiyari lakini ni muhimu ili kuendeleza na kutunza furaha ya kweli na kwa kuzingatia yote hayo ni rahisi kuepuka mahusiano ya haraka na gafla
Namalizia kwa maswali ambayo nahitaji uyajibu bila mimi kusikia
-UNGE PENDA KUONGEZA FURAHA?
-JE UNAWEZA KUISHI BILA MAHUSIANO YEYOTE?
- JE UNAWEZA KUJARIBU KULA,KULALA,KUTOZUNGUMZA NA MTU YEYOTE?
-JE UNAWEZA KUISHI MAISHA YA PEKE YAKO BILA KUTOA WALA KUPOKEA CHOCHOTE KWA MWINGINE?
- JE UNAWEZA KUISHI SEHEMU AMBAYO UNAWEZA KUPATA VITU VYOTE ISIPOKUWA KUMUONA MTU WA JINSIA YEYOTE ?
MWANDAAJI WA MAKALA HII NI LILIANI SETHI