
KILA kinachotokea leo katika maisha yako ni matokeo ya namna ulivyowaza na kutenda kipindi cha nyuma. Maisha ni mipango.
Hata katika uhusiano na mapenzi ni hivyohivyo. Kama hutakuwa mkweli, hutaishi maisha safi na utaonesha picha mbaya kwa jamii, kesho utakutana na majibu yake.
Umakini katika maisha ya uhusiano ni mzuri, kwanza kutakujenga kiakili, moyo hautakuwa na ukakasi maana una msimamo thabiti. Suala la kupenda ni muhimu.
Unaweza kupendwa lakini usipende. Unaweza kuwa na mwenzi wako ambaye mmefunga ndoa kabisa, lakini usiwe na mapenzi naye au pendo likapungua na baadaye kuyeyuka kabisa.
Hifadhi pendo moyoni mwako. Penzi ni uwekezaji. Lazima uwekeze pendo moyoni mwako, ujifunze kuwa katika uhusiano sahihi ili siku zijazo uyafurihie maisha.
Mapenzi hayatakuwa na maana kwako kama huna uwezo wa kupenda. Faragha haitakuwa na maana kwako kama hutakuwa na hamu na tendo lenyewe. Wengi wana tatizo hili lakini hawajajua namna ya kujitibu.